GET /api/v0.1/hansard/entries/1176212/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1176212,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176212/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nataka kukushukuru kwa mwito wako wa kuwaalika ndugu zetu, waheshimiwa wa Kaunti ya Baringo. Vilevile, nikijiunga na wewe, ningependa kuwakaribisha hapa ndani ya Bunge la Seneti ili wajionee utaratibu wa kazi unavyoendelea. Katika Bunge hili letu la Seneti, hakuna kuegemea upande ule ambao unajua inafanya makosa hata kama ni upande wako. Mtu ako na haki ya kusema kwamba upande wangu hauko sawa. Ikiwa upande ule mwingine pia unafanya makosa, huwa pia tunawaambia. Hili Bunge ni lile ambalo wazungu wanaita bipartisan . Ninawakaribisha sana. Najua wamekuwa hapa na wamejifundisha mengi. Cha muhimu kuwakumbusha ni kwamba, walipopiga kura mnamo tarehe 9.8.2022 kumchagua ndugu yangu wakili Sen. Cheptumo, walipiga ndipo."
}