GET /api/v0.1/hansard/entries/1176215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1176215,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176215/?format=api",
    "text_counter": 46,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, wakae wakijua, huko nyumbani ya kwamba, wanawakilishwa hapa ndani ya Bunge la Seneti na Seneta mshupavu zaidi. Namtakia ndugu yangu kila la heri katika juhudi zake za kuleta maendeleo huko nyumbani. Cha pili ni kuwakumbusha wabunge wa County Assembly ya Baringo kwamba wakati wa kampeni umekwisha. Mara nyingi tunaona ni kama tunaenda katika hali ya kampeni lakini mambo ya kampeni sasa yamekwisha. Kazi iliopo sasa ni hao kujitokeza wazi na kusaidia watu wa Baringo ambao waliwapeleka katika hilo bunge. Mimi ninataka kusisitiza tu kitu kimoja. Tuwache kusema upande huu ulishinda na upande huu ulishindwa. Tunajua walioshinda. Kama kulikuwa na mambo mengine, basi hayako hivyo tena. Mambo yalikuweko lakini sasa tumeyawacha. Tumeyaweka nyuma na tunasonga mbele. Kenya ni moja. Kwa hivyo, tunataka kuona maendeleo ya Baringo yakiendelea sawa sawa. La muhimu ni kutunza zile pesa. Tukiwa hapa, tunataka kuona kwamba wameangalia ripoti itakayotoka kwa"
}