GET /api/v0.1/hansard/entries/1176217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1176217,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176217/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kwa muhula huu ambao wapo ndani ya hilo bunge, itakuwa vyema kuona ya kwamba wameweza kutenda kazi, kulinda pesa na kutekeleza wajibu wao katika lile bunge la kaunti. Lazima waone ya kwamba zile pesa hazijatumika kwa njia mbaya na miradi ambayo imewekwa ama imepangwa kufanywa imefanywa ili watu wa Baringo wafaidike na hizo miradi. La mwisho, hatuko katika mashindano ya akili. Kama ni kushindana kwa akili, upande huu pia uko na profesa wa sheria. Tuko na watu ambao wamesoma zaidi na watu washupavu. Ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, ni daktari na upande huu uko na profesa wa sheria. Ndugu zangu wengine kama Sen. Cherarkey, Seneta wa Nandi Kaunti, kijana mshupavu, wamesoma zaidi. Yeye ni mwanasheria. Ukiangalia upande huu, utapata jaji mstaafu na kuna dadangu mshupavu."
}