GET /api/v0.1/hansard/entries/1176638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1176638,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176638/?format=api",
"text_counter": 469,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Maseneta wote katika hii Bunge wamekuwa wakishirikiana kuona kuwa wameenda njia moja mwanzo wa safari hii. Maseneta wametaka kuona kuwa tumefanyia Wakenya juhudi wanazozihitaji katika utendakazi wetu kama Maseneta. Sisi bado hatujafanya kile ambacho Seneti iliyopita ilifanya na ninatumaini kuwa wakati wetu ukifika, tutafanya hivyo. Ninatumaini ya kwamba tutapeleka Bunge la Seneti mashinani. Tumekuwa hapa Nairobi na ingekuwa vizuri tutakaporudi, tupate nafasi ya kuenda mashinani ili Bunge letu la Seneti lijulikane kule mashinani kwa kazi ambayo tunafanya. Hivi sasa, ninaona muda umeenda. Tumekuwa hapa pamoja karibu miezi mitatu au nne na sasa ni wakati wa kuenda mapumzikoni. Ninaunga mkono Hoja hii ya kuenda mapumzikoni ili watu waketi na familia zao, wakisherehekea Krisimasi na kukaribisha mwaka mpya pamoja. Hii ni kwa sababu wengine waliondoka nyumbani na mpaka sasa hawajarudi yapata miezi mitatu ama nne. Ikiwa hauko kwa nyumba yako, basi wewe kama Seneta unajua ni nani anaweza kuwa anafanya kazi hiyo."
}