GET /api/v0.1/hansard/entries/1176767/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1176767,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176767/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia swala hili la janga la ukatili wa kijinsia. Kwa hakika, tunajua kuwa janga hili lipo na limekuwa donda sugu. Watu wengi wamepitia shida hizi na Serikali imetumia njia nyingi kujaribu kupigana na janga hili lakini bado hatujafikia pale tunapotakikana kuwa. Kila kituo cha polisi kinapaswa kiwe na kitengo ambacho kinahudumia mambo ya kijinsia lakini hadi sasa, vitengo hivi havijakuwa na nguvu za kusaidia zaidi. Wamejaribu lakini tunaomba wapewe nguvu zaidi ili tuwe na polisi wa kike watakaokuwa kwenye vitengo hivi ili wasaidie akina mama ambao wanakumbwa na shida hizi za ukatili wa kijinsia. Ningeomba nitoe ushauri kwamba ni kweli akina mama nchi nzima wanakumbwa na janga hili lakini mama wa Lamu anapata shida nyingi zaidi kushinda yule wa Nairobi. Hii ni kwa sababu katika Eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, usafiri ni tatizo kubwa. Lazima mtu atumie mbinu zote za usafiri. Lazima utumie barabara, ndege, piki piki na pia mashua. Tatitzo hili likimtokea mtu wa eneo la Ishakani, itakuwa vigumu zaidi kupata usaidizi kushinda mtu aliye hapa Nairobi. Ningeomba kuwa kwa yote yatakayofanywa, laini ya usaidizi 1195, yaani helpline, iweze kuimarishwa. Laini hiyo husaidia sana kuokoa waadhiriwa wa ukatili wa kijinsia. Ingekuwa muhimu kwa Serikali kuimarisha laini hiyo kwa sababu ukiwa na tatizo, unapaswa kupiga namba hiyo. Nataka Wakenya wanisikize. Unapokumbwa na tatizo kama hilo, kama huwezi kufika hospitalini, piga simu kwa 1195. Namba hiyo ni nzuri na inatusaidia sana. Hata sisi Wabunge tunapopata matatizo, huwa tunawapigia na wanatuelezea jinsi ya kufanya kama hatujui. Jambo linalowatatiza ni kuwa hawana uwezo wa kupata ndege na vifaa vya usafiri. Laini hiyo ikiimarishwa zaidi, itasaidia sana kwa sababu katika kusaidia matatizo haya, wakati mwingine wanapambana na forces na inakuwa vigumu sana. Pengine msichana amepewa biskuti au matunda ya mikebe na anaona kama amefika ilhali anatumiwa vibaya. Wakati mwingine mama akipigwa, inakuwa shida sana kupambana na hizo kesi zote. Lakini, Serikali inaweza kusaidia na kuungana mkono na Safaricom, the Office of the President na United States Agency forInternational Developmen t (USAID). Tunaomba watilie jambo hili mkazo ili kuwe na kitengo maalum cha kipekee cha kusaidia kesi hizi kutoka mwanzo hadi mwisho pale kortini."
}