GET /api/v0.1/hansard/entries/1176769/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1176769,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1176769/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Butere, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Spika. Namimi pia nitajitahidi nizungumze Kiswahili sanifu kama dadangu kutoka Lamu. Kwanza, nakushukuru kama Mwanakamati wa Kamati ya Bunge ya Sheria iliyokabidhiwa uamuzi huu. Namuona Mwenyekiti wangu hapa, sijui kama atapata muda wa kuzungumza lakini kama Mwanakamati, nakushukuru kwa uamuzi wako wa busara sana, haswa tukizingatia sheria. Utapata kuwa Wakenya wengi wamehangaika sana kwa sababu ya kupata sheria ambayo imeletwa bila kupitia Bungeni na kujadiliwa na Wabunge ambao wameteuliwa na wananchi. Tunapaswa tujadiliane ili tuone ni sheria ipi nzuri na ni ipi ambayo itawadhuru wananchi. Kwa hivyo, Mheshimiwa Spika, nakushukuru na pia nashukuru wenzangu ambao wameunga mkono uamuzi huo. Pia, ninaunga mkono uamuzi wako kuhusu mambo ya kijinsia. Jamii ambayo haizingatii kutunga ama kuweka sheria ambazo zinalinda wanawake na akina dada haiwezi ikanawiri. Ninaunga mkono uamuzi huo lakini sisi pia kama wanaume, tunaomba kwamba sheria hiyo ipitishiwe. Hii ni kwa sababu siku hizi, hata wanaume wanapigwa nyumbani. Sio wanawake tu wanaopigwa pekee yao. Wanaume pia wanateseka. Tunataka tuwe na jamii ambayo zinazingatia mambo yananoweza kutuendeleza. Kwa niaba ya Kamati yetu, ninakuunga mkono na kukushukuru kwa uamuzi wako. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}