GET /api/v0.1/hansard/entries/1179929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1179929,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1179929/?format=api",
    "text_counter": 335,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ilikuwa wazi kwamba Prime Minister Wakati huo aliweza kupata stakabadhi na kupewa maagizo ya kwamba kuna mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yangeleta hayo madhara. Hata hivyo, aliamua kuichukua ile ripoti na kuiweka na hatimaye yale madhara yaliwafikia watu wa Jiji la London. Tuko katika taswira sawia hapa Kenya na katika ulimwengu mzima. Tumefumbia macho masuala ya mabadiliko ya nchi. Tunaweka lawama na kutaka kutibu dalili za maradhi na kuyakwepa maradhi yenyewe. Maradhi tuliyonayo ulimwenguni mzima ni kwamba, kuna mabadiliko ya hali ya hewa. Jinsi tunavyo jadili hapa ndani, kuna chembechembe za chuki miongoni mwetu. Kila mtu anavuta upande wake. Tunapovuta sana itakatika katikakati na hakuna faida tutakayopata sisi sote. Wenye kupanda mahindi wanavutia upande wao. Wenye mifugo ambayo inakufa wanavuta upande wao. Nasimama hapa kama Mkenya na ningependa kulizungumzia Bunge hili kama Wakenya sote. Sio ile billioni moja waliopewa wale Wameru kuweza kuongeza faida ya miraa yao. Wala si kejeli wale ambao wamepoteza familia na hata mifugo yao katika hali kama hii. Ningependa tuliangalie suala hili kama Wakenya ambao tutaangamia kwa sababu ya kutaka kuonekana kwenye televisheni zetu ya kwamba tunatetea gatuzi ambazo tumetoka. Hili janga ambalo limetukodolea macho ni la kimataifa, Ni sharti tuchukue mwelekeo ambao utaleta suluhu ya kudumu. Juma lililopita, nilikuwa kule mashinani na nimeanza kampeni yangu ya kupanda miti million moja katika Mkoa wa Pwani. Hii ni kwa sababu nina imani ya kwamba mvua ya kutosha itakaponyesha katika taifa la Kenya, hakutakuwa na haya matatizo ya watu wa"
}