GET /api/v0.1/hansard/entries/1179931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1179931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1179931/?format=api",
    "text_counter": 337,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kupigana na wenzao wa Kitui, kwa sababu wanatafuta lishe ya mifugo yao. Nina imani ya kwamba, wale ambao wamekufa kule Turkana na ile mifugo, wanaweza kupitishwa kwa njia rahisi kwenda kwenye afueni ambapo kuna chakula cha kuweza kulisha mifugo yao. Leo kila mtu analinda gatuzi lake kwa sababu hakuna lishe ya kutosha kwa kila mtu, Kenya, na sio watu wa Turkana pekee. Tukiangalia hotuba amabayo ilizungumzwa na Rais wetu akifungua hili Bunge la Kumi na Tatu, alizungumzia masuala ya ushirikiano baina ya Serikali yetu na mashirika ambayo sio ya Kiserekali ili kuweza kuleta irrigation. Hata alitaja masala ya Kaunti ya Turkana. Ningependa tuipatie nafasi Serikali iweze kuweka mikakati ya kudumu na sio kupea directive ya pesa kadhaa ziende mahali kadhaa na hazitatoa suluhu. Tumekuwa tukipokea pesa chungu nzima kutoka kwa mashirika yasio ya Kiserikali ili kuweza kusaidia hii hali ya ukame. Tunaona baadhi ya watu wakitajirika kutokana na misaada hii lakini bado tunaendelea kukosa mifugo na wananchi wetu wananedelea kukufa. Hakuna kiasi cha fidia kinaweza kuregesha roho za ndugu zetu na mifugo ambao tumeipoteza kwa sababu ya ukame. Ipo haja ya sisi kama Wakenya au sisi waheshimiwa Wambunge tulio hapa kuzungumza kwa kauli moja. Tuache kuficha masuala haya nyuma ya ufisadi. Ufisadi ama cancer ambayo inatuangamiza sisi kama Wakenya, ni ukabila. Tuacheni kuja kwenye hili Bunge kila mtu akivutia upande wa gatuzi lake."
}