GET /api/v0.1/hansard/entries/1179933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1179933,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1179933/?format=api",
"text_counter": 339,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tumepewa appointments za Mawaziri na ningependa Mhe. Rais asisitize yale maneno aliyowaambia kwamba hakuwapa Wizara wasaidie jamii zao ila aliwapa hizi ofisi ili walete marekebisho na suluhu ya kudumu katika taifa letu la Kenya. Bw. Spika wa Muda, Kenya ina wasomi, maji ya kutosha na nguvukazi ambayo inatosheleza sisi kupata manufaa. Jambo ambalo linatuchenga ni sisi hatutaki kukabiliana na donda sugu la ukabila. Tusimame hapa ndani ya hili Bunge na tuzungumze kama Wakenya ambao wanataka kuleta suluhu katika taifa letu. Kwa hayo mengi ama machache, ningependa hatua ichukuliwe kwa haraka ndio kila mtu apande miti katika gatuzi yake. Chakula cha kutosha kikipatikana Mombasa na Kwale, hakuna mtu atakufa Samburu kwa sababu ya ukame. Tutaweza kusaidiana na kile chakula kitapatikana. Nampongeza ndugu yangu lakini naregelea kwamba tusikubali kutibu matokeo ya maradhi. Tuwe wepesi. Afadhali tuchukue muda lakini tutibu maradhi tumalizane nayo kwa ukakimilifu. Asante, ninaunga mkono."
}