GET /api/v0.1/hansard/entries/1180936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1180936,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1180936/?format=api",
"text_counter": 322,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Leo naona mjadala mzuri sana. Sijui kwa nini tuko wachache lakini tutasukuma gurudumu polepole. Nikiangalia mambo ya viwanda, na naangalia kwangu Pwani, ninaona tuna sehemu kubwa na viwanda vingi. Kuna Industries nyingi ambazo zinatengeneza magari, tuk tuk na piki piki. Lakini ningependa kwanza kama inawezekana, Serikali ipunguze ushuru kwa zile materials ambazo zinatumiwa kwenye kuunganisha magari. Kama kweli tunataka kuboresha uchumi wa Kenya na sisi tuna nafasi kubwa sana yakuweza kutengeneza magari yetu ili tuyauze ni lazima pia tufikirie tunatumia mbinu gani. Tukiangalia Mombasa tuko na Simba Corp ambao wanatengeneza Mistubishi Fuso. Tuko na wale ambao wanatengeza… Pia, kuna Tata Motors, Toyota Kenya, Hino Motors, Scania East Africa ambao wanatengeneza Volvo, Bayou Motors na Abson Motors ambao wako sawa kabisa kwa kutengeneza tuk tuk . Vijana wengi wako kule nyumbani, wamesoma, wanajua ufundi na wameenda kwenye vyuo vikuu. Lakini hawajapata mahali wanapoweza kuboresha ujuzi wao ili wainue uchumi wa Kenya. Nikiangalia automobile industry naona kuna nafasi kubwa sana. Badala ya kuleta magari kutoka nje, hapa Kenya tuna vijana ambao wanaweza kupewa vifaa na sponsorship ili waweze kutengeneza magari ambayo ni ya bei nzuri. Pia, sisi tuweze kutoa magari yetu na kuyauza katika mataifa mengine, kama vile tunavyonunua kutoka kwao. Pia, sisi tuboreshe viwanda vyetu ndiyo watoto wetu wapate ajira na waweze kuonyesha ubora wa vile walivyosoma katika college na kutengeneza magari yetu."
}