GET /api/v0.1/hansard/entries/1180939/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1180939,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1180939/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ". Tutaweza kusafirisha na kuuza gari zetu katika mataifa mengine, huku uchumi wa Kenya ukipanda. Mimi kama mama wa Mombasa Kauti nasikitika sana kwa sababu nafasi hii ni nzuri na kama alivyosema Mbunge mwenzangu hii Hoja ilipitishwa mwaka uliopita. Lakini nafurahi kwa sababu niko katika Committee on Implementation. Kwa hivyo, nitakuwa mmoja wa wale ambao watafuatilia kwa kina kuhakikisha kuwa hii policy imeweza kuboresha taifa letu kwa kutengeneza magari kama mataifa mengine na kuwapatia vijana wetu ajira. Napongeza Serikali hili kwa huu mjadala wa leo. Nikiangalia sector ya tuk tuk kule Mombasa utapata wana import kutoka India. Pengine, mtoto wa kiume amehangaika akienda juu an chini ili anunue tuk tuk kwa bei ya laki nne au tano. Lakini Serikali inafaa kufuatilia kwa kina jambo hili la kufungua viwanda. Hasa mimi naomba viwanda hivi viwe ndani ya Mombasa Kaunti. Hii ni kwa sababu mambo mazuri sana yanaonekana kule kwa sababu tayari Scania, Absan Motors, Fuso na Simba Corp wako huko. Ningependa kiwanda kiwekwe kule tuweze kukiboresha kwa kuleta bidhaa kwa bei ya chini ili vijana waweze kusoma na wale ambao wamejitolea pia tuweze kuwapunguzia ushuru ili wale vijana wetu waliosoma college waweze kuboreka zaidi. Zile aina za magari ambazo watatoa naomba Wakenya wanunue ili tuweze kuwa boost hao watoto. Hata kama watatengeneza tuk tuk tutajua watoto wetu wanajimudu na kujaribu. Tuweze kuwa boost baadaye watakuja kuwa bora zaidi. Kenya iko na tajiriba ya kutengeneza vitu vizuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for informationpurposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}