GET /api/v0.1/hansard/entries/1180940/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1180940,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1180940/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Wakati mmoja nilikuwa ninangalia televisheni nikaona mwanaume mwingine kule mashinani ametengeneza gari na linaenda. Nikajiuliza angepata mtu wa kumsukuma kidogo na kumpatia vifaa vinavyofaa basi angeweza kutengeneza gari nzuri zaidi. Kuna mwingine niliona ametengeneza ndege. Mimi nasikitika kwa sababu tuna watu ambao wamebarikiwa sana ndani ya taifa hii lakini, wamekaa mahali wanasikitika pengine hata chakula hawana. Ninaomba serikali ichukue nafasi hii na iweze kutangaza wazi peupe kwamba wale wanaujuzi na wanaweza kufanya kazi katika kiwanda fulani, na kuna walimu watakaowaboresha waende wajiunge ili tuweze kuinua uchumi wa Kenya na vijana wapate ajira waweze kujijenga. Kwa haya machache nashukuru sana. Leo ni siku ya furaha sana kwa vile mjadala huu umetoka kwa serikali. Nina imani viwanda vitawekwa na vijana wataweza kufaidika. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Huyu ni mama Zamzam Chimba Mohammed kutoka Mombasa Kaunti."
}