GET /api/v0.1/hansard/entries/1181131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1181131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1181131/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono taarifa iliyotolewa na Sen. Mumma. Kitambulisho ni haki ya Mkenya yeyote aliyefika umri wa miaka 18. Wakenya katika jamii ya Kisomali na Kiturkana hususan ukitembea sehemu za Kaunti ya Laikipia wanaulizwa maswali mengi sana. Wakitaka kusajiliwa ili kupewa vitambulisho wanaambiwa waje na vitambulisho vya nyanya au babu zao. Inaonekana ni kama hawataki kuwapa vile vitambulisho. Wanaulizwa maswali mengi ilhali wamesomea hapa Kenya kwanzia shule ya chekechea, msingi na sekondari. Yule ni Mkenya. Wakitoa vile vyeti vya kuonyesha masomo yao na pia kadi za ubatizo bado hawapewi vitambulisho. Ikiwa huna kitambulisho hata kupata mkopo katika benki, pia kadi ya NSSF, na National Hospital Insurance Fund (NHIF) inakuwa ni vigumu. Idara ya Usajili Wa Watu inapaswa wafanye usajili wa kuwapa watu vitambulisho uwe rahisi. Si kufanya ule usajili uwe mgumu kupata kitambulisho kwa ndungu zangu wa Kiturkana kutoka Sosian, Rumuruti, Mutara na Doldol. Ni vigumu kama ngamia kupitia kwenye tundu la sindano. Wale wangwana kupata vitambulisho ni vigumu. Tunaomba Kamati itakayoshugulikia mambo haya -Kamati ya Usalama wa Kitaifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa - wasiongee tu ilhali watende kwa sababu hili ni jambo---"
}