GET /api/v0.1/hansard/entries/1181137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1181137,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1181137/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante. Bw. Spika. Waswahili husema Mgala muue na haki mpe. Swala la vitambulisho limekuwa nyeti sana kwa vijana. Mimi ni Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga na kumekuwa na hali ngumu amabapo kijana hana wwazazi. Anapoendea kitambulisho anaambiwa alete cha nyanyake au cha nyanya ya nyanyake. Bw. Spika, ukiambiwa uje na hicho kitambulisho cha nyanyake nyanyako hutakipata. Ni vizuri kama Serikali tunapofanya hesabu za kutoa vitambulisho tusije tukakandamiza wale tunaotetea hapa. Ukienda mahali popote kuajiliwa ata kazi ya mlinda lango unahitajika kuwa na kitambulisho. Ukienda kutafuta pesa ya mahuluku- taabu yani “hustlers” ni lazima uwe na kitambuliso. Ili haki ifikie wale watoto wote ni lazima tujipange tuweze kuwapa vitambulisho. Kwa nini watoto wasipewe zile fomu wajaze wanapofanya mitihani ya Kidato cha Nne ili waweze kupata vitambulisho mwaka huo na wale wengine watapate baadaye. Katika stakabadhi nyingi za Serikali, huwa tunajaza sanduku la posta au physical"
}