GET /api/v0.1/hansard/entries/1181142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1181142,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1181142/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Nami pia naunga mkono hoja hii. Naona kama yote yamesemwa. Ni ukweli vijana wetu wanateseka sana. Vijana wale wamejiunga na vyuo vikuu wanapata shida kujiandikisha kufanya mitihani kwa sababu ya kukosa vitambulisho. Ningeomba watoto wote wapewe vitambulisho kwa usawa. Hii ni kwa sababu, vile imedaiwa, watoto wa upande mwingine huwa wanaonewa kidogo. Waislamu huwa na shida sana kwa sababu wanaitishwa stakabadhi nyingi za kujitambulisha ili wapewe vitambulisho. Utapata ya kwamba watoto wa Kiislamu wanafanyiwa vetting ndiposa wapewe vitambulisho ilhali vijiji vyao na mtaa walipozaliwa unajulikana lakini bado wanasumbuliwa. Namshukuru Sen. Mumma kwa kuleta huu Mswada ambao ni swala nyeti. Watoto wetu wanapaswa kusaidiwa na kupewa vitambulisho wakifika umri. Mwaka uliopita, tuliona ya kwamba kujiandikisha na kupiga kura ilikuwa shida sana. Tulikuwa na idadi kubwa ya vijana ambao hawakuweza kupiga kura kwa sababu ya vitambulisho. Hivyo basi, naunga mkono na naomba Serikali ifanye bidii ili wat---"
}