GET /api/v0.1/hansard/entries/1181271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1181271,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1181271/?format=api",
    "text_counter": 311,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. Veronica Maina. Kusema kweli, huu mjadala unatatanisha sana. Tumeona kweli waschana wetu wameumia, wamenajisiwa, wananyimwa pesa na waajiri wao na kunyimwa chakula, wanapokonywa pasipoti na simu zao ili wasiweze kuwasiliana na Familia zao. Hii ni kisa tu cha waschana wale tunaona. Nashuku pia kuna vijana wetu ambao wanalawitiwa na hawawezi kuzungumziwa kwa sababu wanaona haya, ambao. Vijana pia hueenda kutafuta kazi hizo za nyumbani. Bi. Spika wa Muda, haya ni mateso tumeyaona kwa hawa watoto wetu, dada zetu na ndugu zetu. Kusema ukweli, Serikali ingechukuwa sheria kali dhidi ya mawakala wale wamewatelekeza hawa watoto ama ndugu zetu kule. Lazima sheria iwe kali ili mawakala hao wakamatwe na kuwekwa ndani. Nchi hii lazima iwe na sheria zitakazowezesha kila mtu anayeenda nchi nyingine, afanye kazi na kurudi salama. Ni miaka mingi sana kuona watoto wetu wanarudi wakiwa maiti na wengine wakiwa na ugonjwa wa roho. Juzi, tuliona Mhe. Sonko akiwaokoa wengine wakiwa in a"
}