GET /api/v0.1/hansard/entries/1181277/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1181277,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1181277/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Kila Mara, mimi huuliza kwa nini ni Saudi Arabia peke yake? Kwingine kwaonekana lakini sana ni kwa Saudia na mpaka sasa sijaelewa. Nataka kueleza Seneta Veronica Maina ya kwamba juzi nilikuwa na Balozi wa Saudia aliyerudi tu juzijuzi. Alinipa kadi yake na akanialika kwake kuzungumzia jambo hili. Kitu cha kwanza nilizungumza naye ni hayo mambo ya vijana wetu kwenda kule na kusumbuliwa, kuadhibiwa na kuuliwa. Alisema labda tukae chini kuzungumzia haya mambo."
}