GET /api/v0.1/hansard/entries/1183709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1183709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1183709/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Ahsante, Bw. Spika. Kwanza, ninataka kupatia dada yetu, Sen. Crystal Asige, kongole kwa taarifa hii ya walemavu. Walemavu wako katika aina mbalimbali. Utapata kuwa kuna walemavu wa macho ambao hawawezi kuona, kama dada yetu, Sen Crystal Asige, kuna walemavu hawawezi kutembea, wale ambao hawawezi kusikia na kadhalika. Ni muhimu sana kuona ya kwamba tumeweka mikakati ya kutosha katika hospitali zetu ili walemavu waweze kuwa na njia ya kupitia. Nimekuwa katika hospitali yetu ya Kilifi na sijaona mikakati mzuri ndani ya hospitali ya kuwezesha walemavu kupita katika zile njia bila kupata taabu. Ukienda upande wa ngazi, walemavu wanakuwa na shida wakiwa na magari ya kutembeza kwa mkono ilhali ni lazima wapate matibabu. Utapata ya kwamba wanaenda kumuona daktari wakiwa wamebebwa na watu ilhali walikuja na gari. Gari yao huwa inapandishwa ngazi ndiposa wapelekwe kwa daktari. Kamati ambayo itashughulikia hili jambo lazima izingatie wale watu ambao ni walemavu. Kuna wale watu ambao wanatafsiri; kwa njia ya mikono na wale wanaotafsiri kwa kuongea. Hao pia wapewe nafasi. Itakuwa vyema iwapo walemavu watashughulikiwa katika michezo pia. Stadium ambazo tuko nazo zinafaa zitengenezwe kwa njia ambayo inaangazia mahitaji ya watu walio na ulemavu. Ahsante."
}