GET /api/v0.1/hansard/entries/1183760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1183760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1183760/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ikiwa tunaweza kuambiwa au kuona kwa taarifa ya magazeti ya kwamba kuna magunia milioni kumi ya mahindi ambayo yanangoja kushushwa ili Wakenya waweze kutumia mahindi hayo, tunauliza kitu kimoja: Hawa wakulima wetu ambao tunasema ukulima ni uti wa mgongo, je, sisi kama Wakenya tumewaweka wapi? Hilo ndilo swali muhimu sana la kujiuliza. Hii ni kwa sababu tunaweza kuleta mahindi, yaje hapa na tutakuwa tumeuwa nguvu za mkulima ambaye analima mahindi. Kwa hivyo, ninaona taarifa hii ambayo imeletwa na Sen. Cherarkey hapa ndani, imekuwa ni ya muhimu sana. Ni jambo la kusisitiza kwamba Kamati kama hii ya Ukulima itakayopewa nafasi ya kuchunguza jambo kama hili iweze kuita Waziri na wale watu ambao wame import maanake hii imefanywa na mabiashara. Waulizwe walipewa contract na nani na ilikuwaje hadi wakaleta milioni kumi za hayo magunia ya mahindi. Waje hapa tuwaulize maswali kama kulikuwa kuna ukosefu, ama tender ilitangazwa ama haikutangazwa. Iko namna ngani au ilikuwa vipi ili tuweze kujua na Wakenya wote waweze kujua. Asante."
}