GET /api/v0.1/hansard/entries/1184343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184343,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184343/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Hata mimi nimesimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imetolewa na mwenzangu. Kwa hakika, sisi kama taifa, tuna jukumu la kulinda afya ya Wakenya. Pia tuna jukumu la kuangalia uchumi wa wakulima wa taifa letu la Kenya. Kwanza, nina masikitiko makubwa sana kutokana na matamshi ya Waziri aliposema kwamba iwapo Wakenya wamekuwa wakipata vifo kwa njia tofauti tofauti, basi kupata vifo kupitia vyakula vya GMO hakuna tashwishi. Hayo ni matamshi ambayo ni aibu sana kuwa yametoka kwa kiongozi ambaye ni Waziri katika taifa la Kenya. Kenya tuna taasisi zetu za kisayansi. Tasisi yetu ya KEMRI kwa wakati mmoja waliweza kufanya utafiti wakaona kwamba vyakula hivi ambavyo vinatokana na njia ya GMO vina athari katika maisha ya mwanadamu na pia katika maisha ya wanyama. Vile vile, tukiangalia nchi nyingine za Afrika na hata nchi nyingine katika Uropa, wamepiga marufuku vyakula kama hivyo, yakiwemo mahindi ya GMO. Ufaransa, Italia na Croatia ni nchi ambazo zimestawi sana, lakini hazikubali vyakula kama hivyo. Vile vile, hapa Afrika, nchi ya Zimbambwe imekuwa na ukame mkali sana lakini haikubali kuingizwa kwa vyakula kama hivyo kwa sababu waliangalia janga ambalo litaletwa na vyakula hivyo. Tukiangalia utafiti ya wanasayansi, unasema kwamba vyakula hivyo vinaweza kuleta changamoto za kimazingira na za kiafya kama vile maradhi ya saratani. Vile vile, vinaweza kuleta mambo tunayoyaita “mzio.” Kwa wale ambao hawafahamu, “uzio” kwa kimombo ni"
}