GET /api/v0.1/hansard/entries/1184346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184346,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184346/?format=api",
"text_counter": 381,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Katika mambo haya ya GMOs, hapo nyuma kuna wanasayansi ambao walibadilisha mchele wa kawaida kwa kuongezea vitamini zaidi ndani yake halafu wakauita “mchele wa dhahabu.” Mchele huo katika utafiti umeonyesha kwamba wale walioutumia walipata upofu na hata wengine wakapoteza maisha. Hayo yote ni mambo ambayo yameangaliwa na wanasayansi. Swali la kujiuliza ni kwamba: Je ni utafiti gani wa kisayansi unaothibitisha kwamba vyakula hivyo, yakiwemo mahindi ya GMO, havina madhara kwa afya ya mwanadamu na mnyama yeyote? Tukiangalia utafiti ambao umetolewa, unasema kwamba vyakula hivi vina madhara na si madhara tu ya sasa, bali ya kuendelea. The electronic version of the Official Hansard Report is for informationpurposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}