GET /api/v0.1/hansard/entries/1184347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184347,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184347/?format=api",
"text_counter": 382,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, tukiangazia uchumi, wakulima kule Kitale na sehemu nyingine katika eneo la Bonde la Ufa, wanapata mvua na wanalima mahindi kwa wingi sana. Leo tukileta mahindi ambayo yametengenezwa kwa njia ya uhandisi jeni wa vyakula – hiyo ndiyo tafsiri kutoka Kiingereza ya GMO – wakulima wetu hawataweza kuangaliwa tena sana na Serikali, na pia kutakuwa na utepetevu ambapo wakulima wataona kwamba kuna mahindi mengine ambayo yanaingia nchini kwa bei rahisi na hivyo basi, hakutakuwa na haja ya kuwaangalia wakulima hao. Kama Wakenya, ni lazima tuangazie njia za kukuza vyakula kwa kunyunyizia maji mashamba kutumia mbinu za irrigation, na kuhifadhi maji ambayo yamekuwa mengi kutokana na mvua na mafuriko ili tuweze kuyatumia wakati wa kiangazi. Pia, tunapaswa kuchimba visima na kuhakikisha kwamba wakulima wamepata mbolea na mikopo ili tuweze kupata vyakula vya kutosha."
}