GET /api/v0.1/hansard/entries/1184359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184359/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Kwanza, nampongeza Mhe. Kirwa kwa mjadala huu wa leo. Hali ya wakulima kule mashinani inatamausha na inasikitisha sana. Ni mwaka juzi tu wakulima walipokuwa wakilia wakisema kwamba wana vyakula ndani ya maghala yao lakini vyakula hivyo vinaozea kule. Ningependa kumkumbusha Waziri wa Kilimo kwamba huu ni wakati mwafaka wa kufungua macho na kuangalia Kenya na Wakenya. Ni wakati wa kuwa na msimamo thabiti kuona kwamba Wakenya wanapata chakula kinachovunwa katika sehemu nyingi humu nchini."
}