GET /api/v0.1/hansard/entries/1184360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184360,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184360/?format=api",
"text_counter": 395,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Nikirudi upande wa vyakula vya uhandisi wa jeni, hivyo vyakula vinatolewa nasaba yake ya asilia – yaani ile DNA yake ya mwanzo ambayo imeumbwa na Mwenyezi Mungu. Inatolewa halafu vinaongezwa bakteria na virusi vingine ili kuviboresha. Tangu wiki jana, nimekuwa nikisikitika nikisema watu wangu wengi wa Kaunti ya Mombasa wameadhirika na magonjwa ya saratani. Inasikitisha kwamba ni juzi juzi tu Serikali imetoa mbolea kutoka Russia na kutuahidi kuwa wataboresha ukulima na kupatia wakulima mbegu. Juzi na jana wameondoa marufuku ya kuleta vyakula vya GMO nchini. Sasa tunaambiwa kwamba bandarini Mombasa tayari kuna mahindi ndani ya maghala yanayosubiri kupakuliwa kwa matumizi ya Wakenya. Nasikitishwa sana na Serikali hii. Namkumbusha Rais kwamba Wakenya wamemuamini na kumpa mamlaka ya kuliongoza taifa hili. Ninamuomba awafikirie Wakenya kama alivyo Mkenya. Ikiwa vyakula hivyo vitawaua watu waliompigia kura, basi itakuwa uongozi wake umefeli. Nakumbuka kuna wakati Rais aliwahimiza wakulima wapande avocado. Sijui kama ndiyo ilikuwa mbinu ya kupindua ili tuletewe vyakula hivi. Ninawaza tu kwa sauti. Masikitiko yangu ni kwamba Rais anawafelisha Wakenya. Wakenya wakati huu wanahangaika na hakuna kitu katika mifuko yao. Wanahangaika na akili zao kwa maradhi yanayowakumba. Leo tunawaletea vyakula vitakavyowamaliza kabisa – wafe waondoke katika taifa hili."
}