GET /api/v0.1/hansard/entries/1184361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1184361,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184361/?format=api",
    "text_counter": 396,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, ningependa kuzungumza na Wakenya niwambie kwamba vyakula hivi vitakuja. Mkiona mbiu ya mgambo inalia, jueni kuna jambo. Ningependa kuwashauri kama Mama Zamzam, Mama Kaunti ya Mombasa. Ikiwa kwa njia yoyote ile vyakula hivi vitakuja, basi susieni; msile. Hata enyi wakulima, vile vyenu mlivyopanda, jitoeni kimasomaso msambazie wenzenu. Katika sehemu ya Ganze na Kaunti ya Tana River, watu wanakufa njaa lakini maghala yamejaa mahindi pomoni katika maeneo ya Rift Valley na Trans Nzoia. Kuna Mbunge ambaye amesema hapa kwamba ana takriban kilo 500,000 za mahindi katika ghala lake na hajui atayapeleka wapi wakati watu kule Ganze na maeneo ya Kaskazini Mashariki wanateseka na njaa. Watu nchini Kenya wanakufa kwa njaa. Nataka niulize Serikali na Waziri wa Kilimo ikiwa wamewaelezea Wakenya kuwa kuna chakula tele lakini Wakenya wengine wanakufa njaa? Leo hii mwatuambia tupitishe sera ya kuagiza vyakula vya GMO kutoka mataifa ya nje. Hatuwezi kupitisha sera hiyo katika Bunge hili. Napinga sera hiyo ya Serikali na kumuunga mkono Mhe. Kirwa. Jambo hili haliwezekani katika taifa hili. Tunaweza kuchimba maji katika sehemu ambazo zimekauka na tuwapatie mbolea na mbegu wakulima ili wapande vyakula na Kenya iwe huru. Ikiwa wadudu hawawezi kula chakula cha GMO, juwa kwamba kuna hatari manake kwa kawaida wadudu hutuelekeza sisi binadamu kama kitu ni kizuri ama ni kibaya. Hata wanasayansi leo wamekuwa na hofu ya kusema. Kwa sababu wanajua hawawezi kupata funds wakituambia ukweli, wameficha ukweli na wanasikitika kimoyo moyo. Nawaomba wanasayansi katika taifa hili wajitoe kimasomaso waiokoe nchi hii."
}