GET /api/v0.1/hansard/entries/1184379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1184379,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1184379/?format=api",
"text_counter": 414,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria East, UDA",
"speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru kwa hii nafasi. Mimi sitasema kwamba nina ufahamu wa GMO. Hiyo sayansi mimi siifahamu. Lakini najua kwamba wakulima wetu wengi sana katika maeneo mengi nchini wako na chakula cha kutosha. Wamelima na wanevuna mahindi mengi na vyakula vingine aina mbali mbali na vimo kwenye maghala yao. Wanatafuta tu sehemu ya kuuza. Katika maeneo ninakotoka, yakiwa Kuria East, Kuria West, Kilgoris, Angata Baragoi, Nyamaiya, na kwingineko; mahindi yamejaa katika mashamba hivi sasa. Tuko karibu kuvuna mahindi. Itakuwa ni jambo la ajabu sana ikiwa tutapata kwamba badala ya Serikali kungoja siku mbili au tatu ili iweze kupata mavuno hayo, wananunua mahindi kutoka nje. Wakulima wanapigwa na mshangao kwamba tayari kuna mahindi yamefika katika Bandari ya Mombasa yakingoja kuingia nchini ilhali sisi sote tunajua kwamba ikiwa hivyo, mahindi ya mkulima hayataweza kununuliwa. Kwa hivyo, nimesimama kumuunga mkono Mheshimiwa mwenzangu ambaye ameleta Hoja hii. Tatizo hata sio GMO; tatizo ni tabia mbaya. Tabia mbaya haina tiba. Ni tabia mbaya tu. Hii Serikali inahitaji kutoka katika ule mkondo ambao serikali zilizotangulia zilikuwa zikifuata – tabia mbaya ya kumdhulumu mkulima na mwananchi wa kawaida."
}