GET /api/v0.1/hansard/entries/1185183/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1185183,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185183/?format=api",
"text_counter": 792,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda wakati wangu mwingi umetumika kwa hoja za nidhamu ambazo hazina msingi wa nidhamu yoyote. Bw. Spika wa Muda, Sen. (Dr) Khalwle anazungumzia germs ambavyo ni virusi. Lakini genetics ni viini ambavyo vinaunda mwili wa binadamu ama mwili wa mnyama yoyote ambaye anahusika. Hivyo basi tunasema kwa sasa hatujakuwa na utaalamu katika nchi yetu ya Kenya kuthibitisha kwamba vyakula hivi ni salama kwa wananchi wetu. Kwa sababu hiyo, haitakuwa sawa ile marufuku kuondolewa kwa sababu watu wengi watapata shida ya vyakula ambavyo hawajui vinatoka wapi. Bw. Spika wa Muda, kuna nchi nyingi ambazo zina vyakula hivi na hawana mahali pa kuvipeleka ama kuviuza. Kwa hivyo, hii itaharibia pakubwa wakulima wetu ambao juzi tu walikuwa wanapewa mbolea iliyopunguzwa bei. Ikiwa mazao yao yatakuja kwa wingi, wale watauza mazao yao wapi? Serikali hii ya Kenya Kwanza au ‘Kenya Kwisha’ imetoa fursa ya kutoa mbolea kwa bei nafuu kwa wakulima wa mahindi ili waweze kuzalisha mahindi zaidi ya yale wanayozalisha kwa sasa. Ikiwa tutakubali mazao kama haya ambayo yana utata, wale wakulima wetu watauza mahindi yao wapi?"
}