GET /api/v0.1/hansard/entries/1185320/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1185320,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185320/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": " Nakushukuru Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuongea juu ya jambo la IDPs. Sehemu yetu ya Endebess na Trans Nzoia kwa ujumla, pamoja na sehemu za western zilihusika sana kwa mambo ya watu kuhamishwa kutoka makwao na kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani. Hadi sasa, hao watu hawajafidiwa na Serikali. Serikali ilipotenga pesa ya kufidia, pesa hizo zilifidia wakimbizi wa ndani kwa ndani kutoka sehemu zingine isipokuwa wale wa kutoka sehemu za western na Trans Nzoia. Mpaka wa leo, wakimbizi wa ndani kwa ndani kutoka western na Trans Nzoia wanaendelea kuumia. Mhe. Spika, ninaomba wakati Kamati ya Ardhilhali za Umma itakapokutana, iweze kuita wale Wajumbe wanaotoka sehemu ambazo waathiriwa wanatoka. Ni vyema wakimbizi hao wahusishwe na wasaidiwe na Serikali ili wapate makao na jinsi ya kujisaidia. Ninakushukuru Mhe. Spika."
}