GET /api/v0.1/hansard/entries/1185681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1185681,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185681/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gilgil, UDA",
"speaker_title": "Hon. Martha Wangari",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Naibu wa Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapa kongole wale Wabunge ambao wamepata nafasi kutuwakilisha kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vile wenzangu wamesema, wakienda huko hawaendi kama Azimio au Kenya Kwanza, wanaenda kuwakilisha nchi. Tumeweza kuonyesha kwamba huu uchaguzi haujakuwa rahisi. Tumeangalia mambo kadha wa kadha. Hao Wabunge wamechanganyika. Kuna wale ambao wamekuwa Wabunge kama Mhe. Sankok, Mhe. Falhada, Mhe. Kanini Kega na Mhe. Kering ambao walikuwa katika Bunge la 12. Nilikuwa na Mhe. Sarai Seneti ya kwanza ya 11. Nikiangalia, Mhe. Kalonzo, ana uzoefu kwa sababu amekuwa katika Bunge hilo la EALA kwa muhula mmoja. Lakini la muhimu zaidi ni kwamba kuna mchanganyiko wa umri. Tuna kijana barubaru, Mhe. Karobia, na ambaye hayuko hapa, hakudhani kwamba atapenya. Lakini Mungu naye anapanga mambo yake. Ameweza kuingia na watatuwakilisha na kuonyesha sura nzuri ya Kenya. Kwa hivyo, wakienda kule wakumbuke kwamba wanaweka nchi ya Kenya kwanza. Biashara na utalii inawiri hapa nchini na mambo ya nchi hizi saba yaende vizuri. Kongole zangu. Asante."
}