GET /api/v0.1/hansard/entries/1185705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1185705,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185705/?format=api",
"text_counter": 468,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Mhe. Naibu wa Spika. Nami ningependa kuchukua nafasi hii pia kuwapongeza ndugu na dada ambao wamepata fursa ya kuchaguliwa kuweza kutuwakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki. Kunayo mengi tunayoyahitaji katika hilo Bunge la Afrika Mashariki ili tuweze kuwa na umoja wa Afrika Mashariki. Ni matumaini yetu kuwa wale tuliowachagua watakuwa mabalozi wema katika Bunge hilo. Vilevile, ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza Wabunge wote ambao wameshiriki katika uchaguzi wa leo. Hakika hatukuangalia upande wa Azimio la Umoja-One Kenya ama upande wa Kenya Kwanza. Sote tumeshirikiana kuchagua viongozi ambao watatuwakilisha vyema katika Bunge la Afrika Mashariki. Nisisahau kupongeza Ndugu Shahbal na Binti Odinga kwa zile juhudi zote ambazo wamekuwa wakifanya haswa huko nyuma na wamepata hiyo nafasi kama zawadi kutoka mrengo huo. Vilevile, ningependa kupongeza Wakenya wote na hasa kijana yule ambaye amechaguliwa. Ni kijana mdogo na atatumia ujasiri wake katika Bunge hilo la Afrika Mashariki kuweza kutuunganisha sote."
}