GET /api/v0.1/hansard/entries/1185708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1185708,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185708/?format=api",
    "text_counter": 471,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": "Nawapongeza wote walioingia kwa mchakato huu mzima wa kuomba fursa ya kwenda kutuwakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki. Nawapongeza zaidi walioshinda leo. Kutoka Pwani, ninampongeza sana Mhe. Hassan Omar na Mhe. Shahbal kwa kupata fursa hiyo. Pia, nawapongeza wote hata wale wametoka kwa mrengo wetu wa Kenya Kwanza: Mhe. Sankok, Mhe. Falhada na Mhe. Zipporah. Najua mnaweza kuwa mumetoka mirengo na sehemu mbalimbali, lakini sasa munaenda kuwakilisha Kenya na sisi sote. Muna nguvu na uwezo wa kuweza kutuwakilisha pale. Basi unganeni na muende mutuwakilishe vyema. Tunawatakia kila la heri katika haya majukumu yenu mapya. Mhe. Sankok, pongezi sana. Kama mtu anayeishi na ulemavu, unajikakamua sana, hata kuingia kwa uchaguzi kama huu na kushinda."
}