GET /api/v0.1/hansard/entries/1185722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1185722,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185722/?format=api",
    "text_counter": 485,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii kuwashukuru wote ambao walishiriki katika kinyang’anyiro hiki cha kuwania viti vya EALA. Najua kwamba walikuwa wengi sana—kumi na tano kutoka upande wa Kenya Kwanza na wengine kutoka upande wa Azimio. Nawaambia wale tisa ambao wamepata nafasi hizo kuwakilisha Kenya huko kwamba wao sasa ni sura za Kenya. Mahali mnaenda, mjue kwamba Kenya inajulikana kama Europe ya Afrika Mashariki. Mfikapo huko, msioneshe vitu ambavyo havistahili. Huko mtakutana na Watanganyika, Wanyarwanda, Waburundi, na hata wale watu wafupi wafupi kutoka Congo. Wakilisheni Kenya vizuri. Kuna marafiki wetu ambao wamechaguliwa, haswa wale ambao tumekuwa nao hapa Bungeni. Kama akina Sankok kutoka kaunti yangu, shukrani rafiki yangu; akina Hassan Omar, rafiki yetu ambaye tumekuwa naye; dada wetu, Winnie, binti wa rafiki yetu wa zamani, Raila Odinga; na hata pia kijana wa Kalonzo, shukrani sana. Siku moja nilisema hapa kwamba wawakilishi wa Kenya huko wanatakiwa kuwa watu walio na roho ama wale ambao wanajua Kenya ni nini. Hii ni ili wakituwakilisha huko wajue wanawakilisha Kenya, sio mambo yenu ya kibinafsi. Mnaenda kuwakilisha Kenya yetu. Mkienda huko peperusheni bendera yetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}