GET /api/v0.1/hansard/entries/1185731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1185731,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185731/?format=api",
"text_counter": 494,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi. Moja kwa moja ningependa kupongeza wote tisa waliochaguliwa. Ninawapongeza sana Mhe. Shahbal, Omar na wengine wote. Hapa usawa umefanyika. Vyama vimewakilishwa vizuri, hata walemavu wamewakilishwa kwa hivyo sasa ni wakati wao wa kufanya kazi. Nilikuwa Mwenyekiti wa Regional Integration Committee Bunge lililopita. Nilikuwa nawaomba sana wale waliochaguliwa, ndugu zetu mliochaguliwa, wakienda wajue kuna kazi nyingi. Jumuiya hii iko na taasisi karibu kumi. Katika taasisi hizi kuna mambo mengi ambayo wanafaa kwenda kuyafanya. Taasisi ya kwanza ni Community Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency (CASSOA), East African Community Competition Authority (EACA), East African Development Bank (EADB), East African Health Research Commission (EAHRC), East African Kiswahili Commission (EAKC), Air Steco, Lake Victoria Basin Commission (LVBC), Lake Victoria Fisheries Organisation (LVFO) na Inter-University Council of East Africa (IUCEA). Hapa, nataka kuzungumzia sana Swahili Commission. Kuna mambo mengi ya kufanya. Kuna nchi zingine za Jumuiya ambazo mengi wamesawazisha lakini kwingine bado hayajasawazishwa. Ni jukumu lao wakienda wasawazishe kisawasawa. Yale yamefanywa Kenya na hayajafanywa kule kwingine wahakikishe yamefanywa. Yale yamefanywa kwingine na Kenya hayajafanywa, mhakikishe tumefanya."
}