GET /api/v0.1/hansard/entries/1185734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1185734,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1185734/?format=api",
    "text_counter": 497,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Twalib Bady",
    "speaker": null,
    "content": "mwanzo Mheshimiwa Suleiman Shahbal. Kule Mombasa huwa tunasema Jembe Shahbal. Kwa hivyo, jembe leo limelima. Halafu pia jambo la pili nataka kumpongeza rafiki na ndugu yangu Mheshimiwa Omar na vilevile rafiki yangu Kalonzo. Pia nataka kuwapongeza wote kina Winnie, Falhada, Godfrey na Sankok ambaye tumekuwa naye. Kitu cha muhimu, nimekuwa na Mheshimiwa Shahbal wakati wa kufanya kampeini hizi na moja ya kitu ambacho alisema ni kuna mtu anayeitwa David Lang’at aliekeza kule Tanzania na baada ya kuekeza, akapata shida. Nina imani kuwa hawa viongozi wataenda kule kututetea kwa mambo ya biashara na vile vile kwa mambo ya Muungano wa Afrika Mashariki. Kama Mjumbe wa Jomvu, nawapongeza na kuwatakia kila la heri kule Arusha wanapofanya kazi yao. Asante, Mheshimiwa Naibu Spika. Mungu awabariki wote."
}