GET /api/v0.1/hansard/entries/118596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 118596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118596/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamalwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 148,
        "legal_name": "Eugene Ludovic Wamalwa",
        "slug": "eugene-wamalwa"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii, ili nichangie Hoja hii ya kuidhinisha Sera ya Ardhi iliyobuniwa. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Bw. Orengo, Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na wahusika wote walioshughulika katika kuibuni Sera hii ya Kitaifa ya Ardhi. Bw. Orengo ni kiongozi ambaye amepigania haki na mageuzi katika taifa letu, na tuna bahati sana kama taifa kuwa naye pamoja na Bw. Wakoli na Bw. Rai katika Wizara ya Ardhi. Tunawashukuru kwa kazi ambayo mnafanya. Tunajua kwamba wamefanya kazi ili Sera hii ifike hapa Bungeni. Kufikishwa kwa Sera hii katika Baraza la Mawaziri hakukuwa rahisi. Pia, kupitishwa kwake na Baraza la Mawaziri hakukuwa rahisi. Kwa hivyo, ninatoa heko kwenu na maafisa wenu ambao wamefanya kazi sana kuhakikisha kwamba Sera hii imefika mbele ya Bunge hili, ili ijadiliwe. Ukiangalia historia ya ardhi, utaona kwamba si wengi ambao wameyafurahia mapendekezo yaliyoko katika sera, hasa mabwenyenye ambao wamekuwa na ardhi kubwa. Ardhi kubwa imekuwa katika mikono michache, ilhali Wakenya wengi wakiwa bila ardhi. Tunajua kwamba hii sera ni nzuri. Wenzangu wameichangia hapa na ningependa kuwaunga mkono. Lakini wasiwasi tulionayo ni kama kweli hii Sera itahifadhiwa na Serikali. Tunafahamu kwamba katika Bajeti ya mwaka huu, licha ya Wizara ya Ardhi kuleta ombi la zaidi ya bilioni sita ilipewa bilioni mbili tu. Pia, tunafahamu kwamba mabadiliko ambayo yamependekezwa katika Sera hii yatagharimu zaidi ya bilioni tisa.Wasiwasi tuliyonayo pamoja na Wakenya wengine ni kama pesa hizi zitatolewa. Tunaomba Sera hii na mabadiliko ambayo yamependekezwa yafadhiliwe na Serikali."
}