GET /api/v0.1/hansard/entries/118597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 118597,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118597/?format=api",
"text_counter": 275,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamalwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 148,
"legal_name": "Eugene Ludovic Wamalwa",
"slug": "eugene-wamalwa"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, tukiangalia historia ya nchi hii, tunaona kwamba kwa miaka 46 tangu tupate Uhuru, hatujakuwa na Sera Rasmi ya Kitaifa kuhusu Ardhi. Tunafahamu kwamba wakoloni walipoingia hapa, walipata babu zetu na mifugo na mimea yao. Wakoloni waliwanyangâanya ardhi yao na kuwafanya wapagazi wao na maskwota. Mambo hayo hayakurekebishwa tulipopata Uhuru. Wakenya wachache ambao walikuwa na pesa walinunua ardhi kupitia mpango wa SFT. Kuna Wakenya ambao walibuni makampuni ya kununua ardhi na kuna wale ambao walianzisha mashirika mbali mbali ya kununua ardhi hii. Watu wengi waliokuwa maskwota hawakushughulikiwa."
}