GET /api/v0.1/hansard/entries/118599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 118599,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118599/?format=api",
    "text_counter": 277,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wenzangu wameongea mengi ambayo yamo katika Sera hii lakini mimi ninayetoka katika makao makuu ya maskwota kule Trans Nzioa ningependa kuongea juu ya mambo yanayohusu maskwota. Serikali iliyomtimua mbeberu haikushughulikia swala hili kabisa na Serikali ya pili ilisaidia wachache waliokuwa katika chama tawala. Watu wengi waliopewa mashamba hawakuwa maskwota, bali walikuwa wakuu wa Serikali. Kwa hivyo, tulikuwa na maskwota ambao hawakuwa halisi na hao ndio walifaidika na mashamba ya ADC na KARI. Serikali ya tatu ya Mhe. Kibaki, baada ya NARC kushika ushukani, Kshs400 milioni zilitengwa na kununua mashamba machache katika mikoa ya Pwani na Mashariki. Mwaka wa 2006, Kshs1.5 bilioni ziliwekwa kwa Bajeti na ardhi ikanunuliwa katika Mkoa wa Kati na maskwota wakapewa. Lakini hatujakuwa na Sera Rasmi ambayo inapeana mwongozo kwa swala la maskwota. Nimeuliza katika Bunge hili kwa nini watu wachache walipewa ardhi katika mikoa ya Pwani, Mashariki na Kati na hakuna skwota hata mmoja aliyepewa ardhi katika Wilaya ya Trans Nzoia. Hii ni kwa sababu hatukuwa na Sera inayotoa mwongozo kuhusu swala la maskwota. Tumekuwa na wakimbizi wa ndani sio tu mwaka uliopita bali katika miaka ya 1992 na 1997 lakini hatujakuwa na sheria ama mwongozo unaoshugulikia swala hili. Sera hii inalenga mambo haya. Sera hii inalenga yule aliye mnyonge, skwota na mkimbizi wa ndani. Mimi ni mjukuu wa aliyekuwa skwota katika Wilaya ya Trans Nzoia---"
}