GET /api/v0.1/hansard/entries/118602/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 118602,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118602/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamalwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 148,
"legal_name": "Eugene Ludovic Wamalwa",
"slug": "eugene-wamalwa"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa ninasema kwamba mimi ni mjukuu wa skwota. Labda, Mheshimiwa mwenzangu hajawahi kujua shida za maskwota na ninaomba nipewe nafasi ili nimweleze. Shida ya maskwota ni kubwa sana hasa katika Wilaya ya Trans Nzoia na katika Mkoa wa Pwani. Kuna Wabunge ambao wamechangia swala la maskwota katika Bunge hili. Nilileta Hoja ya kupendekeza tuwe na hazina ya maskwota katika Bunge hili. Katika Bunge la Tisa, Mhe. G.G. Kariuki alileta Hoja ya maskwota na akapendekeza utaratibu wa kuweza kuchunguza na kupata maskwota halisi. Huu ni mchango wa maana sana. Ninamwomba Waziri aangalie michango ya Wabunge walio katika Bunge hili na Bunge zilizopita. Pia Mhe. Koigi wa Wamwere alileta Mswada katika Bunge la Nane na mchango wake ulikuwa mzuri sana na uko katika nakala za Bunge hili. Ningependa Waziri aone ni vipi tunaweza kushughulikia swala hili, ili tutambue maskwota halisi, tuweke hazina ili tuwanunulie mashamba. Pia, inafaa tushughulikie shida ya mabwenyenye ambao wako katika afisi kuu za Serikali na wanaotumia nafasi zao kujinufaisha kwa kujifanya maskwota. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati tulipata Uhuru kulikuwa na Idara ya Kamishina wa Maskwota. Huyo Kamishina alikuwa anaitwa âMzee Zacharia Shimecheroâ. Yeye ndiye alikuwa Kamishina wa mwisho wa Maskwota na ofisi hiyo ikatupiliwa mbali. Kati ya idara ambazo Sera hii inapendekeza kubuni, ninapendekeza tuwe na idara ya kushughulikia maswala ya maskwota ambayo itakuwa na kamishina, ili aweze kushughulikia swala la maskwota na wakimbizi wa ndani. Tukifanya hivi, tutalitatua swala hili kwa muda wa miaka mitano au kumi. Hili ndilo ombi langu. Ningependa kuunga mkono Sera hii na kuwapa wenzangu nafasi."
}