GET /api/v0.1/hansard/entries/1186321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186321,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186321/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emurua Dikirr",
"speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nataka niseme ya kwamba mjadala unaoendelea katika hili Jumba Kuhusu NG-CDF sio suala tunalobidi kuongelea kwa muda. Ninaelewa na tunaelewa kama Wajumbe kwamba saa hii kuna shida nyingi katika serikali, haswa kwa mambo ya pesa na malipo. Lakini, Mhe. Spika wa Muda, hata kama tutaenda kungojea vitu vingine kama majengo na kujenga shule, tungeomba na kupendelea Kiongozi wa Walio Wengi ahakikishe kwamba tumepata pesa ya kwanza ili tuwalipie karo wanafunzi ambao wamejaa kwetu na wako nyumbani. Wanangojea kulipiwa karo. Saa hii tukikaa hapa, jumbe tunazopokea kutoka kwa wanafunzi ni nyingi. Wanauliza ‘tunaenda shuleni lini? Mnatupatia karo lini?’ Naomba na ninaomba kabisa, kwamba serikali kwanza itoe hata kama ni milioni arobaini kwa kila eneo-bunge ili tuwalipie wanafunzi karo. Hii ni tukijua kwamba serikali inaendelea kukusanya na kutafuta pesa nyingine. Lakini, tafadhali, hiyo pesa ilipwe mara moja ili watoto waende shule. Na kuhusu kortini, korti iliamua kuhusu Sheria ya CDF ya 2013, na sio Sheria ya NG- CDF ya 2015. Hakuna mambo ya mtu kutafuta decision ama opinion kwa kitu ambacho"
}