GET /api/v0.1/hansard/entries/118638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 118638,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118638/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Nakushukuru, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi ya kutoa mchango wangu. Katika sehemu ya uwakilishi Bungeni ninayotoka, kulitoka mmojawapo wa waaanzilishi wa Taifa hili, marehemu Paul Ngei. Mheshimiwa Ngei alipokuwa akipigania uhuru, alitoa sauti moja ambayo ilidhihirika katika Kenya nzima, kwamba Mwafrika alitaka haki yake. Msemo aliosema ni kwamba Mwafrika alitaka Uhuru na mashamba yake au uhuru wa Mwafrika na mashamba ya Mwafrika. Jambo hili linadhihirisha kwamba kutoka mwanzo mpaka leo, bei ya ardhi ni ya thamani sana kwa Mwafrika. Bw. Naibu Spika wa Muda, wananchi wamepigana na Mzungu. Lakini hawakupigana na mzungu ili kunyakua meli zake za kupitia kwenye bahari; wala hawakupigana na mzungu ili kupata ofisi zilizokuwa kubwa katika nchi. Lakini walipigana ili kupata ardhi yao. Bw. Naibu Spika wa Muda, mengi yamezungumzwa na mimi nitazungumza kwa ufupi kusema kwamba ulanguzi wa nchi au wa ardhi umekita mizizi kabisa katika nchi yetu. Wenzangu, kwa mfano, mheshimiwa Prof. Olweny, wamesema kwamba sharti kuwe na haki na usawa katika suala hili la mashamba. Nchi imenyakuliwa na waliopewa madaraka. Ni katika nchi hii tu utapata kwamba wale ambao wamekuwa marais wanamiliki ardhi kubwa kiasi cha mkoa mzima, ilhali wananchi wenyewe hawana uwezo wa kukataa jambo hilo kwa kauli moja. Watu wanalala na kuamka na kutembea lakini hilo bado linafanyika nchini humu. Ni muhimu Waziri wa Ardhi kutambua kwamba ni rahisi kutunga sheria lakini kuzitimiza ni jambo jingine – hapo ndipo kuna kazi. Sheria zilizopo sasa hazisemi Rais achukue karatasi na kutia sahihi eti amempa mtu fulani ekari 10,000 za ardhi huku wananchi wengine wakikosa mahali pa kuishi. Ni jambo la aibu sana kuona kwamba leo katika nchi hii, kuna watu wanaoishi kando kando ya barabara na hali kuna wale ambao wana ardhi kubwa. Bwana Naibu Spika wa Muda, ningemsihi Waziri wa Ardhi kufanya kazi yake. Shida ya Wakenya ni kutotii sheria. Wao wanatumia ofisi walizopewa kuhifadhi sheria kuvunja sheria za nchi. Namwomba Waziri afanye awezavyo, ili katika kila sehemu ya uwakilishi Bungeni atenge sehemu za makaburi. Jambo ambalo limechangia vile vile mizozo ya mashamba ni sehemu za makaburi. Ningemwuomba ahakikishe kwamba ametenga sehemu za kuzika watu. Sisi Wakristo na wale wanaozingatia desturi za Mwafrika, itatuchukuua muda kuiga mtindo wa kuchoma mili. Sharti tuishi tukijua kuna sehemu zilizotengewa makaburi. Kuhusu cheti cha kumiliki ardhi, ni jambo la aibu sana kuona Serikali inawashika watu na kuwaweka ndani eti inadai kodi. Ni Serikali hiyo hiyo inayotoa vyeti vya kumiliki ardhi. Utapata Serikali ikitangaza kwamba cheti fulani cha ardhi hakifai. Tunashindwa kuelewa kuna Serikali ngapi. Je, tuna Serikali mbili; moja ya kupeana cheti na nyingine ya kutwaa cheti hicho? Ijapokuwa nahimiza Serikali ilinde vyanzo vya maji, naishtumu Serikali kwa kufurusha watu kutoka sehemu ambazo Serikali yenyewe iliwapa watu vyeti vya kumiliki ardhi. Hivi sasa, Serikali inawafurusha bila kuwapa pahali pengine pa kuhamia. Ni lazima cheti kilichotolewa na Serikali kitambuliwe na kuheshimiwe na Serikali yenyewe."
}