GET /api/v0.1/hansard/entries/118640/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 118640,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/118640/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hiyo ndiyo njia tu ya kuonyesha kwamba mtu huyu ana haki ya kumiliki ardhi kikweli bila kudhulumiwa na wengine. Bwana Naibu Spika wa Muda, ni aibu kuona kwamba watu wanajenga kiholela katika miji yetu mikuu. Mtu anaamka na kujenga nyumba popote atakapo. Sheria zimevunjwa! Bw. Waziri, umeambiwa hapa na mhe. Wetangula kwamba kuna Waziri mmoja huko Nigeria ambaye alivunjavunja majumba ya kifahari yaliyomilikiwa na Marais. Mimi nakuhimiza uangalie kule sheria imevunjwa na utekeleze haki. Ilinde sheria ya nchi yetu kikamilifu ili vizazi vijavyo vijue kwamba sheria yapaswa kulindwa na kufuatwa. Mwisho, kuna ardhi zilizotupu, kwa mfano, hapa Machakos karibu na sehemu yangu ya uwakilishi. Kuna watu ambao wana ekari 5,000 hadi 20,000 ilihali kando yao, kuna wananchi ambao hawana chochote. Watu hawa wote wana vitambulisho sawa. Haijalishi mtu huyu ni mwanajeshi, Rais, Waziri ama nani. Mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu, watu hawa wote ni sawa na nchi hii ni yao. Wale watu wanaomiliki mashamba makubwa makubwa na hawayatumii, hawakuzaliwa na Mungu na wale wengine wakazaliwa na shetani! Tunataka mashamba hayo yachukuliwe na Serikali, kisha iwauzie wananchi hawa ambao hawana mashamba, ndiposa tuweze kulima na kupata mazao ya kulisha watu wetu. Haifai hata kidogo hali ilivyo sasa. Ikiwa, kwa mfano, tutakuwa na Marais wanane na mikoa yetu ni minane, kisha kila Rais amiliki ardhi kiasi cha mkoa mmoja, je, tutaishi wapi? Wao watakuwa wanamiliki nchi nzima na sisi wengine tutaishi kwenye upepo. Angalia haya mambo, Bw. Waziri. Ninayo imani Mungu atatulinda."
}