GET /api/v0.1/hansard/entries/1186449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186449,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186449/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Mimi naunga mkono Hoja hii ya kupanda miti. Mimi ni mwanachama wa Kamati ya Mazingira na Mali Asili. Ni jukumu letu kuona ni vipi tutaongeza upandaji wa miti, haswa katika zile sehemu ambako mvua inanyesha saa hizi. Viongozi wetu, tusipande miti kando ya barabara kuu peke yake. Tupande miti katika barabara zote zikiwemo zile ambazo ziko katika wodi. Wajumbe wa mabunge ya kaunti wa wodi wahusishwe. Kamati za mazingira ziko katika serikali kuu na serikali za kaunti. Kwa hivyo, wajumbe wa mabunge ya kaunti wahusishwe pia ili zile barabara ndogo katika wodi zetu pia zipandwe miti. Tukifanya hivyo, tutafikia kile kiwango kikubwa cha upandaji wa miti milioni kumi na zaidi kwa muda mchache."
}