GET /api/v0.1/hansard/entries/1186450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186450,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186450/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": "Pia, nataka kuzungumzia jambo moja, ijapokuwa limepita. Nilikuwa nimekuhusisha na NG-CDF pale mwanzo. Kiongozi wa wengi Bungeni alizungumzia tu upande wa zile pesa kuhusiana na maeneo Bunge peke yake. Nataka kuzungumzia pesa za wawakilishaji wa kike ndani ya kaunti zetu 47. Sisi hatuna kesi mahakamani kuhusiana na National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). Zimecheleweshwa. Ni ombi langu tuone ni vipi Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina ya Taifa, Prof. Ndung’u, atatoa hizo pesa. Sisi pia tunalipa karo za shule. Tuna miradi na watu wetu. Kina mama, vijana na ndugu zetu wanaoishi na ulemavu wanahitaji usaidizi. Wanategemea viongozi wa kike, yaani Women Representatives, kama mimi kutoka Kilifi ili wasaidike. Kwa vile hatuna kesi kama NG-CDF, tunamuomba Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina ya Taifa apeane hizo pesa kwa haraka kabla hatujaenda likizoni, ndio tuone vipi tutakavyosaidia."
}