GET /api/v0.1/hansard/entries/1186455/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186455,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186455/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Hata mimi nilibonyeza kidude kitambo ili nizungumzie swala la NG-CDF, lakini sikupata nafasi. Labda uniruhusu dakika moja niseme ni vyema waachilie hizo pesa kwa sababu zinasaidia wengi sana kule mashinani. Umaskini ulioko kule mashinani ni mkubwa sana. Hata watu wakiambiwa wapeleke mia mbili ya chakula shuleni inawashinda. Ni vyema sana Serikali iachilie hizi fedha ambazo zinasaidia watu maskini. Hali ni ngumu na kazi hakuna. Watu wanategemea hiyo pesa. Kwa hivyo, sioni sababu ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina ya Taifa kusema kwamba ataenda kutafuta ushauri kwa Mkuu wa Sheria. Hii ni kwa sababu NG-CDF haijashtakiwa. Sioni sababu ya kufanya hivyo. Pengine anachukua muda alafu aziwachilie fedha hivo. Sisi tunahimiza kwamba ni jambo muhimu."
}