GET /api/v0.1/hansard/entries/1186604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186604/?format=api",
"text_counter": 410,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
"speaker_title": "Hon. Mpuri Aburi",
"speaker": null,
"content": " It is okay. Asante Mhe. Spika wa Mda kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, jambo la mashamba katika nchi yetu ya Kenya ni mbaya zaidi. Kwa mfano, ukiangalia upande wa Meru, kuna pahali panaitwa Timau ambapo watu wana zaidi ya 4,000 acres . Na wale wamepakana nao wako na only 20 points . Yule jamaa ambaye ako na ekari zaidi ya 4,000 utapata anafanya kilimo cha kuuza mazao nje ya nchi. Wengine wanapeleka mazao yao Afrika Kusini na wengine Netherlands. Wakaazi wa pale ndio wanaendelea kuumia. Hoja hii ninaiunga mkono kwa sababu inaangalia maslahi ya watu ambao hawana uwezo wa kuwa na shamba kubwa. Mara mingi, watu wanahangaika na kutaabika kwa sababu ya mashamba. Kwa hivyo, ninasema kwamba hii ni Hoja ambayo inashughulikia mwananchi wa kawaida aliye chini na hajiwezi. Hoja hii ikipitishwa, Kenya nzima itakuwa na usawa kwa sababu kuna wengine ambao wako na shamba lakini hawailimi. Wengine wana wanyama katika mashamba hayo na ndiposa ninasema kama wao hawataki kuwa na haya mashamba, watozwe ushuru mkubwa zaidi. Ushuru huo lazima uwe juu zaidi ili iwe vigumu kulipa. Hivyo, watawauzia Wakenya Wengine. Kuna mashamba yasiyo ya kununuliwa ambayo yalipatwa kwa njia isiyo ya halali na wale waliomo Serikalini. Wao hawajali wale wanaohangaika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}