GET /api/v0.1/hansard/entries/1186607/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186607,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186607/?format=api",
    "text_counter": 413,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
    "speaker_title": "Mhe. Mpuru Aburi",
    "speaker": null,
    "content": " Sijatumia lugha mbili ila nimetumia lugha moja. Ninasema ya kuwa Serikali inayo tawala sasa iweke vioo vya pembeni katika gari lao ili iangalie inapotoka na inapoelekea. Kuna wale walipata mashamba kwa njia isiyofaa na wenzao wakitaabika. Ukiangalia upande wa Tana River, Mombasa, Molo na Kwale, kuna watu walio na mashamba makubwa ilhali jirani zao wanataabika. Ndiposa ninasema kwamba ningependa kuumuunga mkono aliyeleta Hoja hii ili watu wapendane, wasikizane na tuwe na umoja. Katika nchi yetu ya Kenya, walio na pesa ndio wataishi vyema na wasio nazo watataabika. Walio na mashamba makubwa wayagawe ama wawauzie wale wana uwezo wa kuyanunua. Mhe. Spika wa Muda, ninashukuru na ninaunga Mkono Hoja hii."
}