GET /api/v0.1/hansard/entries/1186690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186690/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ninaunga mkono Taarifa hiyo. Ni vizuri hao wanariadha waliobobea watwikwe majukumu mengine. Wanaweza kuwa mabalozi ambao watapeperusha bendera yetu ughaibuni. Ni jambo la kuvunja moyo kwamba huwa tunawapongeza wakati huu lakini baadaye, utapata wanaishi maisha ya uchochole. Ni vizuri kwamba hata baada ya wao kufanya vizuri, wapewe mafunzo ya utumizi na uwekezaji wa hela zao. Wakiwekeza hela vizuri, watazitumia katika siku zao za usoni wakati ambapo hawataweza kukimbia tena ama kufanya biashara zingine."
}