GET /api/v0.1/hansard/entries/1186793/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186793,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186793/?format=api",
    "text_counter": 140,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Taarifa kutoka kwa Sen. Osotsi. Kama tunavyojua, nchi yetu ilikumbwa na janga la Korona na vile vile, baada ya hapo kukawa na wasiwasi kutokana na uchaguzi uliofanyika mnamo 9th Agosti, 2022. Yote hayo yaliadhiri uchumi, hususan utalii kwa sababu utalii unapendelea mazingira ambayo yako na utulivu na usalama. Bw. Spika, sasa kwa vile uchaguzi umekwisha na uchumi umeanza kufukuka, Wakenya wengi, mashirika na wafanyikazi wa serikali wamepata fursa ya kwenda kwenye mikutano, ili kuweza kujadili miradi na maswala mengine ya kuendesha Serikali. Hili jambo la kuzuia mikutano kufanyika katika hoteli itaadhiri pakubwa uchumi na biashara ya utalii kwa sababu utalii mwingi unaofanyika sasa ni wa mikutano, ama “ conference tourism.” Ukienda Mombasa hivi sasa, utapata hoteli kama Pride-Inn, White Sands na Serena zimejaa. Vile vile, hoteli nyingi kule Naivasha pia zimejaa kwa sababu mashirika mengi na wizara za serikali zimechukuwa fursa hii kufanya mikutano katika hoteli zile. Bw. Spika, mwaka huu ni kama umeshapotea. Kwanza, tulikuwa tunapona kutokana na janga la korona. Baadaye, kukaingina kampeni, ambapo watu wengi hawakuwa tayari kuondoka manyumbani kwao, kwenda kutembelea mahoteli kwa"
}