GET /api/v0.1/hansard/entries/1186797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186797,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186797/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi hii. Nachukua nafasi hii pia kumshukuru Sen. Osotsi, kwa kuleta Taarifa hii. Utalii ni kitega uchumi kikubwa cha Jamhuri ya Kenya. Mimi natoka katika Kaunti ya Lamu iliyopo katika Jumuiya ya Pwani. Sisi watu wa Lamu tunategemea sana utalii. Utalii ni jambo ambalo Lamu imejivunia kwa muda mrefu sana na sekta hiyo imeweza kuajiri vijana wengi katika Kaunti ya Lamu. Kwa hivyo, naunga mkono yale wenzangu wameweza kusema ya kwamba utalii ni jambo ambalo Serikali inafaa ichukulie na uzito sana, ikizingatiwa kwamba utalii umeajiri vijana wengi sana katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bw. Spika, kwa muda mrefu imejulikana ya kwamba utalii umebobea zaidi huko Lamu. Serikali inapochukua hatua ya kupinga mikutano katika mahoteli, itakuwa inaua uchumi wa nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, tuko na hoteli nzuri sana kule Lamu, kama vile Majlis Resort, Mahrus Hotel, Peponi Hotel na Jonathan Hotel. Hoteli hizi zote ni za kifahari. Huwa naudhika na kusikitika sana wakati ambapo mikutano mingi inafanywa Mombasa na Naivasha na huku Lamu hatupati wageni kutoka Seneti ama Serikali haitumi viongozi kuenda kule kufanya mikutano. Bw. Spika, ningependa Maseneta na Wabunge waende kustarehe kule Lamu kwa sababu ni mahali pa mandhari mazuri. Wakienda kule, watajivunia kuwa Wakenya. Naomba tuunge mkono jambo hili. Namwomba Katibu wa Seneti na Manaibu wake wakubalie Maseneta kwenda Lamu. Nachukua nafasi hii kuwaalika waheshimiwa wenzangu tarehe 24 hadi 26 ambapo tutakuwa na Cultural Festival ambayo itajumuisha mataifa mengi kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa hivyo, naomba Waheshimiwa na viongozi wengine wa Serikali wafike kule ili wajivinjari katika Kaunti ya Lamu. Bw. Spika, nawahakikishia Maseneta wote ambao watafika kule kuwa nitasimamia chakula cha mchana. Pesa za matumizi watakazopewa hapa wahakikishe wanatumia kule, ili watu wa Lamu pia wajivunie kupata wageni kutoka Seneti. Asante sana."
}