GET /api/v0.1/hansard/entries/1186823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186823/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii fursa kuchangi Taarifa iliyosomwa na Seneta wa Kilifi Sen. Madzayo kuhusu shida iliyowakuba watu wa Kijiji cha Pindukiani, Kilifi Kaunti. Kisa kilichowapata watu wa Pindukiani kinaadhiri Wakenya nchi nzima. Watu tofauti wamepatwa na madhila haya kwa sababu wa mizozano ya mashamba. Migogoro ya ardhi hapa nchini imeongezeka. Kwa sababu ya mabwenyenye ambao wanatumia njia za mkato na zisizo za kisheria kunyakua ardhi za wananchi ambao ni maskini na kuwaacha katika shida na tabu nyingi. Nilikuwa mwanachama wa Kamati ya Ardhi katika Bunge la 12 na sasa katika Bunge hili la 13. Kuna Taarifa nyingi ambazo zinakuja kwenye hii Kamati kwa sababu ya migogoro ya ardhi. Kamati hii itachuguza tukio hili lililowapata watu wa Kijiji cha Pindukiani. Tutalivalia njuga na kuwasaidia wananchi wa Pindukiani. Watu wengi wamebomolewa nyumba zao. Watu wanaopata shida wakati wa ubomozi kama huu ni akina mama na watoto. Tumetembea mitaa mingi. Kwa mfano, mwaka wa 2020 tulienda huko Diani na tukaona watu waliyobomolewa nyumba bila kufuatwa kwa sheria. Wakati nyumba zinabomolewa lazima tueke ubinadamu kwa sababu wananchi maskini watataabika zaidi. Kamati hii ya Ardhi, Mazingira na Maliasili tumekuwa na Taarifa kuhusu shamba la watu wa Mswambeni maeneo ya Voi. Kampuni ya Bata ilipewa shamba kule Voi lakini haijenga kiwanda cha viatu. Baada ya miaka miwili walishurutishwa na lease ya shamba kuwa wasiuze lile shamba. Hivi sasa mahakama imepitisha kwamba watu zaidi ya 3,500 watolewe kule Msambweni, Voi. Ni lazima tuvalie njuga suala hili kwa sababu ni jukumu la Serikali kupeana makaazi kwa wananchi. Tunataka Serikali inunue shamba na kuwapa watu wa Mswabeni hati miliki. Tutalivalia njuga hili suala la Voi na la Kijiji la Pindukiani. Sisi kama Kamati ya Ardhi tumefanya mapendekezo kwamba Serikali kupitia kwenye Settlement FundTrustee Board. Lile shamba linunuliwe ili wale wananchi wa pale Voi wapewe. Na hili suala la Pindukiani, pia wananchi kule wanafaa kupewa shamba hilo. Tutapendekeza hivi tutakapoenda Kilifi kufanya uchunguzi zaidi. Lile shamba linafaa linunuliwe na Serikali ili wale watu wa Pindukiani wapewe kama vile shamba la Waitiki kule Mombasa, Serikali ilinunua na kuwapa wananchi hao makaazi. Nashukuru sana kwa fursa ya kuunga mkono Taarifa hii."
}